Breaking News
Loading...
Monday, 9 May 2016

NONDO YA 19- HATUENDI KWA SABABU TUNAVIJUA ZAIDI VIKWAZO

01:33




Wengi tumekwama mahali ambapo hatutaki kukaa na hatuwezi kutoka. Tunaweza kudhani kuwa kuna mtu au watu, mfumo, chama cha siasa, hali ya uchumi nk ambavyo ndivyo vinavyo tuzuia kusogea.

Ukweli ni kwamba kizuizi kikubwa kipo kwenye akili zetu.

Tunaviona zaidi vikwazo kuliko fursa.
Tunazijua zaidi changamoto kuliko fursa.
Tunajua zaidi ugumu uliopo kuliko uwezekano.

Kibaya zaidi tunavitazama zaidi hivyo vikwazo, ugumu na changamoto kiasi kwamba hatuwezi kuona mlango mpana wa uwezekano uliopo.

Wana  saikolojia wana sema You produce what you think about most of time.

Unaweza kushangaa yale mambo ambayo uliwahi kuyaona na ukaona ugumu na kuto kuwezekana, leo amekuja mtu mwingine na akafanya kama ambavyo wewe ulitaka kufanya na  amefanikiwa.
Usijisikie vibaya sasa, hakikisha wakati ujao hufanyi kosa kama hilo tena.
Jizoeze kuangalia upande unao utaka. Hakuna fursa inayokuja ikiwa na upande mmoja tu. Kwa hiyo licha kutowezekana unako kuona, ukiangalia vizuri utaona uwezekano ndani yake.

Kila mara tafuta upande unaoutaka na uuangalie.
If you think about impossibilities that bis exactly what you are going to produce..

Be positive…. Think positive

©Grant Sumaye
+255 763 449 749
Facebook/ Grant sumaye
Instagram: Grant_s.s


0 comments:

Post a Comment

 
Toggle Footer