NONDO NAMBA 11- JIFUNZE KUIONA KESHO TANGU LEO.
1.
Waliofanikiwa sana ni wale ambao waliweza kuona leo tangia jana na kufanya jambo jana kuhusu leo.
uwezo wa kuona mbali ni sifa ya muhimu sana kama unahitaji mafanikio.
Kuwa na mawazo ya zaidi ya leo ni jambo la muhimu.
kuiona pekeyake haitoshi, bali pia kuwa na uwezo wa kufanya jambo leo kwa ajili ya kesho.
Unahitaji kuwa na uwezo wa kuamua na kufanya . wengi wanajua kabisa jambo la kufanya leo kwa ajili ya kesho yako lakini wanakosa nguvu ya maamuzi katika kulifanya.
ni vema ukajenga nguvu ya nia ili uweze kushinda vizuizi vinavyo kuzuia kuijenga kesho yako.
Usikubali kuishia kuishi leo. kesho pia inakuhusu

0 comments:
Post a Comment