Breaking News
Loading...
Wednesday, 20 April 2016

NONDO YA. 14 – KUWA JIRANI NA WATU WANAOKUPA SABABU YA KUENDELEA.

12:40

NONDO NO. 14 – KUWA JIRANI NA WATU WANAOKUPA SABABU YA KUENDELEA.

Siyo kila mtu anaelekea unapoelekea wewe. Ambatana na watu wanaolekea unapo elekea wewe. Ukitumia muda mwingi na watu ambao hapo ulipo wao ndo wameshafika, basi lazima watakufanya na wewe uwe umeshafika.

Mbaya zaidi ni pale unapo jaribu kung’ang’ana na watu ambao wanarudi ulipo toka. Nakuhakikishia lazima watakurudisha nyumba.

Huwezi waepuka kabisa watu wa aina hiyo kwenye maisha, labda kama utatafuta dunia nyingine.
Ninacho maanisha ni kwamba, tafuta watu ambao watakupa sababu ya kuendelea hata pale unapojisikia kusimama ama kurudi nyuma.
Tafuta watu watakao kuvuta ukizembea
Tafuta watu watakao kutia moyo ukikata tama.
Watakao kuhamasisha ukilegea moyo,
Watakao kukumbusha ukisahau.
Watafute watu wa namna hiyo na utumia muda wako mwingi zaidi kuwa nao kuliko lile kundi la kwanza.



0 comments:

Post a Comment

 
Toggle Footer