Breaking News
Loading...
Saturday, 16 April 2016

NONDO YA 12. UNAWEZA KUFANYA KARIBU KILA KITU

23:20



1   NONDO YA 12.  UNAWEZA KUFANYA KARIBU KILA KITU


Kuna watu watakufa wakiwa masikini kwa sababu wanaona hakuna kitu wanachoweza kufanya kikawafaa kiuchumi.

Kila wanachoambiwa wanaona hawawezi.
Kila wazo wanalopata wanaona hawawezi.

Hawawezi biashara, hawawezi kufuga, hawawezi kulima hawawezi chochote.

Wanajiona wana uwezo ama ujuzi mdogo kuliko wenginge.

Ukweli ni kwamba

Unaweza kufanya karibu kila kitu ambacho ni cha kawaida kama tu utaamua kujifunza.
Kila kitu ambacho wapo watu wanaoweza , basi upo uwezekano wa wewe kuweza.
Tofauti ya wale wanaoweza na wasioweza ilianza pale wale wanaoweza walipoamua kuweza na wakaamua kujifunza.

Unaweza hata kufanya upasuaji wa moyo kwa binadamu kama utaamua kujifunza. Wanaorusha ndege nao kuna siku walikuwa kama mimi nawewe, sema tu waliamua kujifunza.

Wanaofanya bishara kubwa kuna siku walikuwa kama mimi na wewe, sema tu kuna siku waliamua kuweza na wakaanza kujifunza.

KIla unayemtamani uwezo wake naye aliwahi kuwa kama wewe.

HATA WEWE UNAWEZA, UKIAMUA KUWEZA

0 comments:

Post a Comment

 
Toggle Footer